Saturday, November 12, 2011
MEYA WA ILALA ASAINI MKATABA NA BENKI YA TIB KWA AJILI YA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA KISUTU
Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana nyaraka za mkataba wa awali na Mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Investment Bank baada ya kutia saini makubaliano ya awali ya manispaa ya Ilala kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la kisutu. Manispaa ya Ilala sio tu ndiyo ya kwanza kwa halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na TIB,Bali pia mradi huu utakuwa unamilikiwa kwa 100% na halmashauri tofauti na miradi ya ubia. Hii imekuja kuunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa Jakaya M Kikwete aliyeiongezea mtaji TIB kwa maendeleo ya nchi yetu. Ujenzi unategemewa kuanza mapema mwakani na mpango huu utaendelezwa kwenye masoko mengine kutimiza mpango wa meya Silaa wa kuwa na masoko makubwa na ya kisasa kama njia mojawapo ya kuondoa machinga mitaani,kukuza ajira na huduma.
Labels:
kimataifa
